Monday, October 23, 2017

SEMINA YA UJASIRIAMALI NDANI YA JIJI LA MWANZA.

Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, Umeendelea na Jitihada zake za kupambana kwa namna ya Kuwakomboa kiuchumi vijana wa Ccm Kupitia Fursa Mbalimbali za Ujasiliamali zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Mwanza ili kuhakikisha vijana wa Ccm wanakuwa na Uchumi Imara kupitia fursa hizo zitakazo waongezea uwezo wa kujiajili na kupata kipato Cha kukidhi Mahitaji yao.Katibu wa Vijana mkoa wa Mwanza Bi Mariam Amiry,Akiambatana na Baadhi ya Macada Kindakindaki wa Ccm,Comred Alfonce Kaligilwa,Servant Davis,Comred Eliud,Conso na Dada Mgen  Secretary wake wamefanya kikao maalum na Makatibu wote wa vijana wa Kata ya Ilemela walioteuliwa ili kuwashirikisha fursa zenye tija na Manufaa ya Vijana wote wa Chama Cha Mapinduzi juu ya namna ya kupata nafasi ya kushiriki Mafunzo ya Ujasiliamali (Nadhalia na Vitendo) jinsi ya kutengeneza Sabuni,Kufanya ufugaji wa kisasa,kilimo Cha Kisasa,Kutengeneza Keki,Namna ya kufanya Mapambo,kuanzisha Biashara, namna ya kupata masoko ya Biashara n.k kwa mda wa Siku 3 mfululizo.Picha Hakikabidhi Ticket Mia Mbili kwa Katibu wa Vijana Ilemela Comred Amos, na Mkiti Wa Vijana Ilemela Aliyeteuliwa Comred Faida ili ziwafikie vijana wa Ccm watakaoshiriki katika kupata Mafunzo Hayo yatakayo anza tare24-27.2017 CCM MPYA, TANZANIA MPYA, ITAKUJA KWA KUFANYA KAZI KWA WEREDI NA KWA MOYO WA KUJITOA KWA FAIDA YA TAIFA LETU.VIJANA WA MKOA WA MWANZA TUNAISHI IMANI HIYO KWA VITENDO.





No comments:

Post a Comment