Serikali ya China imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 20 kwenda kusoma masuala ya gesi na mafuta nchini humo.
Akizungumza
katika hafla ya kuwaaga wanafunzi hao, Katibu wa Wizara ya Nishati,
Hamis Mwinyimvua amesema lengo la ufadhili huo ni kuhakikisha Watanzania
wanajengewa uwezo wa kushiriki katika uendelezaji wa rasilimali ya
mafuta na gesi ipasavyo.
Amesema
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, iliingia makubaliano na
Serikali ya China kutoa ufadhili wa fani ya mafuta na gesi kwa ngazi ya
Shahada ya Uzamili na Uzamivu ambapo kwa mwaka huu wameongeza hadi wale
wa shahada ya kwanza ambapo tangu programu hii ianzishwe wanafunzi 100
wamefadhiliwa.
“Niwapongeze
Watanzania wenzetu waliopata ufadhili kwa mwaka huu, haikuwa kazi
rahisi na maombi yalikuwa mengi ila wao wamechaguliwa katika nafasi hizo
na mjue mnaenda kuwakilisha nchi hatimaye mlete ujuzi nchini.
“Tunaishukuru
serikali ya China tumekuwa tukisaidiana katika mambo mengi hasa hili la
ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, ufadhili huu ni mhimili muhimu
katika nchi yetu kuwa na wataalamu wa kutosha katika sekta ya nishati
ambayo ni injini ya kufikia katika Tanzania ya Viwanda,” amesema.
Kwa
upande wake muwakilishi wa Balozi wa China, XU Chen amesema serikali
yake iliamua kutoa ufadhili huo kwa Tanzania kwa kipindi cha miaka
mitano ili kusaidia kupata wataalamu katika sekta ya nishati jambo
ambalo litaimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
“Tanzania
ni nchi yenye utajiri wa mafuta na gesi ila hawana watu wenye taaluma
ya kutosha jinsi ya kuvumbua rasilimali hizo na hii ndiyo sababu
imetufanya tutoe ufadhili huu na tunafuraha kuona ushirikiano wa nchi
hizi mbili unakua,” amesema Chen.
No comments:
Post a Comment