Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Leo
amekabidhi sadaka ya futari Kwa taasisi za Elimu zilizopo ndani ya
Jimbo hilo ikiwemo shule ya sekondari Bwiru wavulana, Chuo Cha Mipango
na shule ya sekondari Bwiru wasichana ambapo Sukari Kilo 110 zilitolewa
Kwa kila taasisi, Mchele Kilo 110 kwa Kila taasisi, Tambi na Tende Ili
wanafunzi waislamu waweze kupata futari katika kipindi hiki cha mwezi
mtukufu wa Ramadhan
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya sadaka hiyo, Katibu wa Mbunge Ndugu Kazungu
Safari Idebe amesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela amekuwa na
utaratibu wa kuungana na waumini wa dini ya kiislamu kila mwaka
unapofika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kutoa sadaka ya futari
ili kusaidia waumini hao waweze kufunga kwa salama na amani
'..
Mhe Mbunge alitamani kuwepo yeye mwenyewe katika zoezi hili, Lakini
kutokana na majukumu ya kitaifa aliyopewa ameshindwa ingawa siku za hivi
karibu alianzisha yeye mwenyewe zoezi hili Kwa kutoa sadaka hii katika
vituo vya watoto yatima, Wajane, Misikiti, Wazee na Watu wenye uhitaji,
Na leo sisi wasaidizi wake akaamua tumuwakilishe kuendelea alipoishia..'
Alisema
Aidha Ndugu
Kazungu amefafanua kuwa Serikali na nchi Kwa ujumla ina mategemeo
makubwa Kwa wanafunzi hao na kuwaasa kuutumia mwezi huu mtukufu kuombea
taifa na viongozi wake wakiongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
sanjari na kuongeza kuwa taifa lolote lenye hofu ya Mungu lazima liwe na
Maendeleo
Kwa upande
wake Mkuu wa shule ya sekondari Bwiru wasichana Mwalimu Mektilda Shija
mbali na kumshukuru Mbunge huyo amesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela
Mhe Dkt Mabula amekuwa mtu wa msaada katika shule yake na si mara ya
kwanza kufika kutoa misaada kwani mara kadhaa amekuwa akishirikiana nao
katika kutatua kero mbalimbali zinazoikabili shule hiyo hivyo kuwataka
wanafunzi wake kumuombea hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa
Ramadhan
Hawa Japhari ni
mwanafunzi wa kidato Cha Tano anaesoma masomo ya mchepuo wa sayansi
(CBG) katika shule ya wasichana Bwiru amempongeza na kumshukuru Mbunge
Mhe Dkt Angeline Mabula Kwa msaada alioutoa pamoja na kumuombea Kwa
Mungu Ili kidogo alichokitoa aweze kuzidishiwa