Thursday, April 28, 2022

RAMADHAN CUP 2022 KANKONO AJIVUNIA VIPAJI VYA VIJANA VILIVYOKO MKOA WA MWANZA

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Dennis Nyamlekela Kankono amesema Mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kuwa na Vijana wengi wengi wenye vipaji Mbalimbali kama Soka,Filamu,Waimbaji,Waigizaji n.k.

"Mkoa wa Mwanza katika Soka tunaitwa Brazil sababu kutoa wachezaji wengi kama Calvin Yondani, Enry Joseph, Mrisho Ngasa, Mwinyi Kazimoto n.k."

aneyasema katika Mchezo wa Nusu fainali ya pili ya Mashindano ya Ramadhani Cup ambayo yamedhaminiwa na Mhe. Stanslaus Mabula (MB) bado yameendelea leo na ambapo Mgeni Rasmi katika nusu fainali hii alikuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza Ndg. Dennis Nyamlekela Kankono.

katika Mchezo huo Timu ya Mwanza mjini imeibuka kidedea kwa ushindi wa magoli mawili kwa moja.

Fainali ya Ramadhan Cup itakuwa Ijumaa ya tarehe 29/04/2022.

USIKOSE! 







No comments:

Post a Comment