Saturday, April 23, 2022

KATIBU WA UVCCM (W) YA ILEMELA AENDELEA KUCHANJA MBUGA

 Mapema Leo katibu wa UVCCM( W) ya Ilemela Ndugu HAMISI MAGOHE  ameendelea na Ziara yake katika kata ya Kahama na Shibula


Katika ziara hiyo aliyoambatana na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Ndugu Edwine Kabide ,katibu huyo amezidi kutoa maelekezo mablimbali yanayohusu uchaguzi na zoezi la uchukuaji na urejeshwaji wa fomu katika matawi 

Akizungumza na vijana pamoja na makatibu wa CCM wa matawi mbalimbali ,katibu amewakusha Viongozi wa jumuiya ya vijana kuhakikisha kuwa wanasimamia kanuni ,muongozo na taratb mbalimbali za Chama na jumuiya yake ili kufanikisha zoezi la uchaguzi kwenda Kwa haki na uwazi 

Pamoja na mambo mengine ,katibu huyo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha vijana kujitokeza Kwa wingi na kutoa Hamasa Kwa wananchi katika maeneo Yao kujitokeza Kwa wingi ili waweze kuhesabiwa pindi zoezi hilo la sensa litakapofika 

#Kazi iendelee
#Ilemela kazini
#Viva Vijana Viva 
#Alipo Mama ,vijana tupo







No comments:

Post a Comment