Thursday, June 28, 2018

MWENYEKITI UWT MAGU AWAFUNDA WAZAZI NA VIONGOZI


Katika ziara ya kamat ya utekelezaji wilaya ya Magu Leo katika kata ya kitongosima, mwenyekiti wa UWT amewaambia wazazi kuwapunguzia kazi watoto wa kike majumbani name badala yake wawapatie muda wa kujisomea kama ilivyo kwa watoto Wa kiume jambo ambalo litaongeza ufaulu wao kielimu.

Pia amewataka wanawake wajishughulishe na kilimo cha kisasa,biashara ndogondogo na mambo mengine ya maendeleo ili kupunguza utegemezi na kuleta maendeleo katika jamii.

Pamoja na hayo mwenyekiti amewahimiza wataalamu Kama watendaji Wa kata, mabwana mifugo na mabwana shamba kutoka nje (field )ili wawasaidie wananchi kwa ushauri na vitendo  pia kuwapa elimu ya kutosha na sio kukaa maofisini.






No comments:

Post a Comment