Wednesday, June 27, 2018

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO WILAYANI NYAMAGANA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg John Mongella amezindua mpango endelevu wa BIMA ya Afya Kwa Watumiaji wa Vyombo vya MOTO wakiwa Madreva na Kondakta wilayani Nyamagana. Mpango huu umeandaliwa na Chama Cha Madereva wa Daladala na Makondakta Mkoa wa Mwanza MWAREDDA Kwa kushirikiana na taasis ya mfuko wa hifadhi za Jamii NHIF. Katika halfla ya Uzinduzi wa BIMA ya AFYA kwa Madereva wa Daladala na Makondakta 31 Wamepatiwa BIMA ya afya nakulenga kuwafikia wengine 311 kisha madreva wote. 

Akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bi Mary Tesha Mkuu wa wilaya ya  Nyamagana amepongeza Chama Cha MWAREDDA kinachowaunganisha Madreva pamoja na Kondakta WA Daladala katika kutetea masilahi yao.  Amesema  ushirikiano taasis ya NHIF  na vyama vya Watumiaji wa vyombo vya MOTO ni wenye tija na wa kuigwa hususani  kuwajali wanachama wake wakiwa kazini na kupatiwa BIMA ya Afya. Amewahasa madreva na kondakta wote kuhakikisha mpango huu kuwa endelevu na Uwe jumishi kwa waendeshaji na Watumiaji WA vyombo vya Moto vyote. 

Naye Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula kupitia Mwakilishi wake Ndg Ahmed Misanga amepongeza  jambo hilo LA kuigwa ambako lipo katika mpango Kazi wa serikali kuhakikisha kila Mwananchi anakuwa na BIMA ya Afya. Hivyo Amewaasa Watumiaji wa vyombo vya Moto kuhakikisha wanakuwa salama nyakati zote wa kizani, kuzingatia uadirifu kadharidha kujali afya zao kwa kukata BIMA ya Afya pamoja na BIMA ya Vyombo vyao watumiavyo ili kuepuka hasala inayoweza kujitokeza wakati wa ajari. 

Naye Ndg Mpangala  kaimu Maneja NHIF mkoa wa Mwanza amewahasa Dreva na Kondakta 31 waliopata BIMA hizo za Afya kutokuzigawa Maana kwa kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na Sheria za BIMA na ikibainika mtoaji na mtumiaji wa ziada wote watakuwa makanisani hatia. Kadhalika amemwambia mgeni rasmi kuwa wanamkakati endelevu kuwafikia wanachama 311 kisha kuenea Kwanzaa Watumishi wa vyombo vya Moto Wote Dara Dara pamoja na Boda Boda.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi katibu MWAREDDA wa amesema Madreva na kondakta wengi wangepanda kupata huduma ya BIMA ya afya Lakini waajiliwe wao kukosa kuwaajili katika ajira rasmi kumewanyima HAKI hiyo wengi wenye kupokea posho.  Wameiomba serikali kulisimamia hili ilipambwa haki hiyo ya msingi Iweze kuzingatiwa.

Naye mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi La Polisi kituo cha Buzuruga amewaasa Madreva  kuwa makini sana kutojihusisha na mambo ya uhalifu. Pia kutoajwaajili taarifa Mara moja katika vyombo vya Usalama endapo watabeba au wataona abilia anajihusisha na uhalifu pamoja na Biashara aunt matumizi ya Mihajarati.

Inetolewa na,
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿






No comments:

Post a Comment