Saturday, December 16, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA AGAWA KATIBA ZA CCM KWA MAKATIBU KATA

Mwandishi Yusuph Ludimo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt  Angeline Mabula leo  amegawa Katiba za Chama Cha Mapinduzi kwa Makatibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi kwa Kata zote za Jimbo la Ilemela huku akiwataka kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kufuata Katiba na taratibu za Chama

' Leo tumegawa Katiba kwa Kata zote zitakazosaidia utekelezaji wa majukumu ya kila siku kwa viongozi wetu wa kwenye Kata hasa makatibu, Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba kuzingatia Katiba na taratibu za Chama watakapokuwa wanatekeleza wajibu wao ...' Alisema


Aidha zoezi hilo limefanyika mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya  wilaya hiyo kilichoketi kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi wa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo itakayodumu kwa miaka mitano mpaka tamati yake mwaka 2022 ambapo Ndugu Masanja Caroline, Magera Salehe na Sengo Kajala waliibuka kidedea

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela




No comments:

Post a Comment