Inakutaarifu kuwa kesho Tarehe *21/01/2018* utafanyika mkutano wa kuzindua kampeni za Ubunge na Madiwani Jimbo la SIHA utafanyika kesho *saa nane (8:00) mchana* uwanja wa *KKKT Karansi.*
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa *Mh. MWIGULU NCHEMBA* na viongozi wengine wa Kitaifa.
Kwa taarifa hii viongozi wa *UVCCM* kutoka ngazi zote mnahimizwa kuhudhuria na kuwapa taarifa wanachama wote wa *UVCCM* na *CCM* na kuwahamasisha kuhudhuria katika Mkutano huo!
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kwa namna tutakavyo pokea!
Ahsante!
*IMETOLEWA NA IDARA YA UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI MKOA KILIMANJARO!*
*TUKUTANE KAZINI*
No comments:
Post a Comment