Mwandishi Yusuph Ludimo
Wazee wa Kata ya Nyamanoro Jimbo la Ilemela wamemtuma
Mbunge wao na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe
Dkt Angeline Mabula kupeleka salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli kwa jitihada kubwa
anazozifanya katika kuwaletea maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wazee hao mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi kata ya Ibungilo Ndugu Dotto Erasto Mangu amesema kuwa wazee
wa Nyamanoro wanaridhishwa na jitihada kubwa zinzofanywa na Mhe Rais
katika kulitumikia Taifa hasa udhibiti wa mianya ya upotevu wa
rasilimali za nchi ikiwemo mapato na madini, utekeleaji wa miradi
mikubwa ya ujenzi wa reli ya kisasa, ununuzi wa ndege mpya na za kisasa,
upanuzi wa uwanja wa ndege wa mkoa Mwanza na barabara yake ya kutoka
mjini kati kwenda uwanja wa ndege inayopita katika kata yao, kurudisha
nidhamu ya kazi kwa watumishi wa Umma, uboreshaji wa huduma za afya na
ongezeko la bajeti yake.
‘… Mheshimiwa mbunge wazee wa Nyamanoro wanasalamu zao
tunakuomba uzipeleke kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli, Kamwambie
tunamshukuru sana kwa kututetea sisi wanyonge lakini pia jitihada
anazozifanya za kulijenga taifa hili, Kasi yake inaonekana wala
haijifichi na tunampongeza kwa hekima anazozitumia katika kukisaidia
chama chetu leo tunaona wapinzani wanavyomiminika kurudi kwetu, CCM
wanaiamini wananchi, Wenyewe mmeona kupitia uchaguzi huu mdogo
uliokwisha majimbo yote tumeshinda kwa zaidi ya 90%…’ Alisema
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Dkt Angeline
Mabula amewahakikishia wazee hao kuzifikisha salamu hizo huku akiwaomba
kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Mhe Rais na wasaidizi wake na
kuwataka kuwa wazalendo kwa kulitumia vizuri zoezi la urasimishaji
makazi litakalofika ukomo mwezi Juni 30, 2018 kwa kulipia upimaji na
hati miliki.
Mbunge wa Ilemela amehitimisha ziara yake ya utekelezaji wa
Ilani kwa kata hiyo ya Ibungilo ziara iliyohusisha jumla ya kata 14 za
Kayenze, Sangabuye, Bugogwa,Shibula, Kahama, Buswelu, Nyamhongolo,
Nyakato, Mecco,Buzuruga, Nyasaka, Kawekamo na Ilemela, kwa awamu ya
kwanza, Na kuahidi kumalizia kata 5 zilizobaki kufikisha jumla ya kata
zote19 za Jimbo lake mara baada ya kumalizika kwa vikao vya uwakilishi
bungeni mjini Dodoma.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa naOfisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.01.2018






No comments:
Post a Comment