Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameungana na waheshimiwa
wabunge wengine wakiongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Tulia Ackson pamoja na mke wa aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya nne Mhe Salima
Kikwete katika kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Buyungu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
Mhe Mwl. Kasuku Samson Bilago kilichotokea juzi katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Saalam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Aidha kwa siku ya Kesho Jumanne ya Mei 29, 2018 wabunge
wote watapata fursa ya kuaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Bunge
Jijini Dodoma.




No comments:
Post a Comment