Mnamo
tarehe 18/06/2018 majira ya saa 13:15hrs mchana katika barabara ya
Usagara – Kigongo Ferry maeneo ya Kingongo Ferry kijiji cha kigongo
Ferry kata ya Bukumbi tarafa ya usagara wilaya ya misungwi mkoa wa
mwanza, gari no. T.581 ARL aina ya scania bus kampuni ya SABCO
iliyokuwa inatokea Mwanza kuelekea Msalala wilaya ya Nyan’gwale mkoa wa
Geita likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Idd Omary miaka
40, Mnyamwezi, mkazi wa Mkuyuni- Mwanza, liiligonga ofisi ya Ferry na
kusababisja kifo kwa Zabroni Malando, miaka 37, Msukuma, mfanyabiashara
na mkazi wa Sengerema, aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu
katika hospitali ya bukumbi.
Aidha
pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa watu kumi (10), wanaume sita
(6) na wanawake wa nne (4), wote wapo katika hospitali ya Bukumbi
wakiendelea kupatiwa matibabu.
Aidha
kati ya hao majeruhi mahututi wapo watatu ambao ni Idd Omary, miaka 40,
dereva wa gari lililopata ajali, Ibula Raphael, miaka 34, msukuma,
mkulima na mkazi wa Busolwa na Sophia Lugihila miaka 45, msukuma,
mkulima na mkazi wa msalala na wote wamepelekwa hospitali ya Sekouture
iliyoko Mwanza kwa matibabu zaidi.
Chanzo
cha ajali ni kuferi kwa breki za gari hali iliyopelekea gari hilo
kugonga ofisi za ferry na kusababisha kifo na majeruhi.
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bukumbi kwa ajili ya
uchunguzi na utambuzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu
wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina msaidizi wa polisi Mkadamu
Khamisi Mkadamu anatoa pole kwa wote hususani kwa ndugu na jamaa wa
marehemu wa ajali hiyo, tunawaombea kwa mwenyezi mungu awape nguvu
katika kipindi hiki kigumu. Aidha pia tunawaombea majeruhi wapone haraka
ili waweze kuendelea na kazi.

No comments:
Post a Comment