Jeshi
la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa wameahidi kushirikiana katika
miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kupitia mashirika yake ya Magereza
Corporation Sole na SUMA-JKT.
Hayo
yamejiri wakati wa ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
Phaustine Kasike alipomtembelea Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja
Jenerali Matin Busungu ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za
kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa
mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.
Katika
mazungumzo yao, wakuu hao wa taasisi hizo muhimu nchini wameonesha
utayari wa ushirikiano katika miradi ya ujenzi pale taasisi moja
inapokuwa na miradi mikubwa inayoweza kuhitaji utaalam au nguvu ya
kuweza kushirikiana.
Aidha,
Meja Jenerali Busungu amesema kuwa JKT lipo tayari kulikopesha
matrekta Jeshi la Magereza wakati litakapokuwa limekamilisha mpango
wake kilimo cha kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa kama
ilivyoelekezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli.
“Namshukuru
sana Meja Jenerali Busungu kwa kuonesha utayari wa kushirikiana na
Jeshi la Magereza, kilichobaki ni kujipanga na kuanza utekelezaji mara
moja”. Amesema Jenerali Kasike.
No comments:
Post a Comment