Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa NSSF pamoja na Kampuni ya Mwanza Huduma wameamua kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kumkabidhi mifuko mia nane na themanini ya Saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na tano kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ndugu Matson Mwakila amesema kuwa NSSF ni mfuko wa jamii wenye sera ya kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka kwa kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii ikiwemo miradi ya afya, elimu, michezo na mengineyo yenye umuhimu mkubwa kwa jamii, Kupitia ombi lililowasilishwa na taasisi yake ya mbunge wa jimbo la Ilemela ya The Angeline Foundation kuamua kusaidia jamii hiyo
‘… Sisi NSSF tutaendelea kuunga mkono serikali na viongozi wake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kumaliza kero na changamoto zinazoikabili jamii, Pia niwaombe watu wengine kutushirikisha wakati wowote watakapohitaji msaada wetu na mara zote tutaendelea kufanya hivyo …’ Alisema
Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Huduma ndugu Zully Nanji mbali na kumhakikishia ushirikiano mbunge huyo amesema kuwa kitendo cha kumuunga mkono mbunge huyo si mara ya kwanza na ataendelea kufanya hivyo ili kumaliza kero na changamoto zinazoikabili jamii
Akihitimisha makabidhiano hayo mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amewashukuru wadau hao kwa kumuunga mkono huku akiahidi kuitumia saruji hiyo kwa kufyatulia tofali zitakazotumika kukamilisha maboma ya majengo ya madarasa, zahanati au ofisi za taasisi za umma kulingana na mahitaji huku akiwaomba wananchi na viongozi kuendelea kushirikiana.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga, Kaimu mkurugenzi Daniel Batare na viongozi wengine mbalimbali.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
No comments:
Post a Comment