Monday, July 23, 2018

NYAMAGANA YAHAKIKISHIWA MAJI YA UHAKIKA

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Hamidu Aweso hivi leo amewahakikishi uhakika wa upatikanaji maji wakazi wa Nyamagana katika kata zote 18 ifikapo 2019.

Mhe Aweso akizungumza na wakazi wa Nyamagana kata ya Mkolani katika mkutano wa hadhara, amesema serikali ya CCM imedhamiri kufikisha  maji safi na salama kwa wananchi wote sanjari na kampeni yake ya kumtua Ndoo mwanamke kichwani. Hadi sasa tuweka mkakati wa ujenzi wa matank ya maji kwa ukanda yatakayowezesha kata zote 18 zinafikiwa na maji safi na salama.

Mhe Aweso akijibu maswali ya wananchi ya Papo kwa Papo amebainisha  Kukabiliana na changamoto ya Maji Safi na Usalama tayari serikali ya  awamu ya  tano imewezesha ujenzi wa matank yenye uwezo wakuhifadhi Lita 1,000,000  tank mmoja linaweza kuhifadhi ujazo wa  Lita 800,000  na lingine lita 200,000 na tayari mkandarasi anaendelea na Kazi. Na lingine linatarajiwa kujengwa lenye uwezo wa kuhifadhi lita 1,200,000.  Kadharika ameagiza MWAUWASA kuweka mkakati wa kuhakikisha kati zote zenye uhaba wa maji kufikiwa na maji wakati wote wa ujenzi wa matank mapya.

Mbunge wa Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula amemshukuru Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kufika na kuzungumza na wananchi wa Nyamagana. Amemwambia Mhe Naibu Waziri Jiji la Mwanza linazaidi ya wakazi 400,000 na linakadiliwa kuhudumia watu zaidi ya 800,000 kila siku. Amesema Tank na mtandao wa maji wa Capripoint ulikuwa umeandaliwa kuhudumia wakazi 150,000 hivyo amepongeza serikali kwa mkakati wake madhubuti uliouweka Nyamagana utakao wezesha Nyamagana inakuwa na uhakika wa maji.

Katika mkutano huu wa hadhara kadhari mwenyeviti wa wenyenyeviti wa CHADEMA amejiunga na Chama Cha Mapinduzi

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana





No comments:

Post a Comment