Wednesday, September 26, 2018

DKT ANGELINE MABULA ASHIRIKI MAZISHI VIFO VYA AJALI YA MELI YA MV NYERERE.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula Leo amewasili Kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe kuungana na viongozi na wananchi kwaajili ya kushiriki mazishi ya Vifo vilivyotokana na ajali ya meli ya Mv Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018.

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula amewaasa wananchi kuwa wamoja na wenye utulivu katika kipindi hiki cha maombolezo sambamba na kuweka mbali tukio hilo la ajali na mambo ya siasa wakati Serikali ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo kupitia kwa Tume ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Mkuu Mhe Kasim Majaliwa ikiongozwa na Mkuu wa majeshi mstaafu Mhe George Waitara.



' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga'

Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
23.09.2018.



No comments:

Post a Comment