Mwili
wa Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita
unatarajiwa kuzikwa Jumatano Septemba 19, 2018 kijijini kwao Kibaoni,
Ifakara mkoani Morogoro.
Guninita
ambaye jina lake linabaki katika orodha ya wanasiasa wenye uwezo wa
kutenda kile wanachoamini alifariki dunia jana Septemba 13, 2018 katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mdogo
wa marehemu, Gerald Guninita amesema mwili wa kaka yake utachukuliwa
MNH Jumanne asubuhi, misa ya mazishi itakayofanyika nyumbani kwake
Tabata Kimanga.
Amesema, awali Guninita alikuwa anasumbuliwa na kwiwi, kiungulia na baada ya vipimo alibainika kuwa na uvimbe tumboni.

No comments:
Post a Comment