Thursday, September 20, 2018

Mhe DKt ANGELINA MABULA AWAPA POLE WANA UKEREWE ..!



Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula anatoa pole kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongela, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe Boniphace Maghembe na wafiwa wote wa  ajali ya Meli ya MV Nyerere iliyotokea Siku ya Leo   Septemba 20, 2018 katika Visiwa vya Ukara wilayani  Ukerewe.

Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula anawaombea heri majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupata nafuu ya haraka ili warejee katika majukumu yao ya kila siku ya ujenzi wa taifa.

' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga.

Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
20.09.2018.


No comments:

Post a Comment