Serikali
imeeleza kuwa uwekezaji wa mishahara kwa wafanyakazi nchini ni jukumu
la mfanyakazi mwenyewe kwa kuwa mshahara ni mali ya mfanyakazi hivyo
anaweza kuutumia kwa kuwekeza au kuto kuwekeza.
Hayo
yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti
maalum Mhe. Mwantum Dau Haji, aliyetaka kujua Serikali inasema nini
kuhusu uwekezaji wa mishahara kwa watumishi wa umma na kuwepo kwa
ucheleweshaji wa mishahara kwa Watumishi wa Umma..
Dkt.
Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa upande wake inawalipa mishahara
wafanyakazi wake kwa wakati kwa kuzingatia waraka wa Hazina namba 12 wa
mwaka 2004 ambao unaitaka Serikali kulipa mishahara kabla ya tarehe 25
ya kila mwezi.
“Kumbukumbu
za malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma zinaonesha kuwa, kuanzia
Julai 2017 hadi Agosti 2018, watumishi walilipwa mishahara yao kati ya
tarehe 20 na 24 ya kila mwezi hivyo napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu
na umma kwa ujumla kuwa hakuna ucheleweshaji wa malipo ya mishahara kwa
watumishi wa umma” alieleza Dkt. Kijaji.
Aidha
Serikali imekuwa ikiwatendea haki wafanyakazi wake katika upandishaji
wa madaraja na kila mwaka wafanyakazi hupandishwa madaraja.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

No comments:
Post a Comment