Rais
Dk. John Magufuli ameahidi kulipa madeni ya mishahara ya wafanyakazi wa
'Marine Service' jijini Mwanza ambao wanadai shilingi bilioni 3.7 na
atawalipa ndani ya wiki huku akiwaonya kufanya kazi kwa juhudi na
ipasavyo.
Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo akiwa jijini
Mwanza kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Meli mpya na
Chelezo katika Ziwa Victoria, ambapo ujenzi huo utagharimu shilingi
Bilioni 88. 76.
''Mimi nitawapa hizo bilioni 3.7 ndani ya wiki
mbili, sasa ole wenu msifanyekazi tena mtazitapika, nawaambia kabisa huu
sio muda wa kubembelezana lazima tubanane kwa sababu tumechelewa'',
ameonya Rais Magufuli.
Wafanyakazi hao wanadai malimbikizo ya
mishahara ya takribani miezi 27 ambapo Rais Magufuli ameeleza
kuridhishwa na mwenendo wa uendeshaji wa sasa wa Marine Service chini ya
Kaimu Mkurugenzi Erick Hamis.
Rais yupo ziarani katika mikoa mitatu ya Mwanza, Simiyu na Mara ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

No comments:
Post a Comment