Kaimu
meneja wa Kampuni ya Meli (MSCL) Erick Hamis amesema kwamba ujenzi wa
meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 yenye tani 400 utatoa ajira
250.
Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa
ujenzi wa meli hiyo mpya na ukarabati wa meli nyingine za MV Viktoria na
Mv Butiama na ujenzi wa Chelezo.
Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula amesema kwamba baada ya meli ya Mv Bukoba kuzama usafiri ulikuwa wa shida.
“Tunatumia fursa hii kukushukuru(Rais Magufuli) kwa jitihada zako na sisi tutakuunga mkono,’’amesema.
Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amesema tukio hilo ni dhahiri kwamba Rais ana dhamira kwa anayoyasema.
Alisema
kwamba Rais aliposema anajenga reli kutoka Mwanza alikuwa pia
amedhamiria na kwamba miundombinu hiyo itasaidia kukuza uchumi wa Kanda
ya Ziwa.
“Wapo watu ambao hawataki kuamini kinachofanyika lakini ukweli ndio huo,’’amesema.

No comments:
Post a Comment