Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya
Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ili kuhakikisha kuwa Kilimo kinakua kwa
asilimia 6 kwa mwaka kuendana na malengo ya Programu Kabambe ya
Maendeleo ya Kilimo Barani Afrika (CAADP).
ASDP
Awamu ya pili inatekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka
2017/18 hadi 2027/28 imekijikita katika kuleta mageuzi ya mtazamo
uliopo wa kilimo cha kujikimu kufikia uendeshaji wa kilimo kwa mfumo wa
kibiashara.
Aidha
ASDP awamu ya pili imeweka kipaumbele kuendeleza mazao ya kilimo
yakiwemo mazao makuu matano ya biashara (pamba, tumbaku, korosho, kahawa
na chai) kwa kushirikisha wadau mbalimbali, hatu inayolenga kutimiza
malengo ya Tanzania kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda
ifikapo mwaka 2025.
Wakulima
nchini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa
miundombinu mizuri na umbali wa masoko, hivyo hukwaza wakulima
kusafirisha mazao yao hadi mahali pa kuyauzia na wengi wao kujikuta
wakiuza mazao yao kwa walanguzi na wasafirishaji kwa bei ya chini.
Mara
nyingi wakulima hupunjwa kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi za soko,
au kutoelewa vipimo halali vya uzito na ujazo na wafanyabiashara wasio
waaminifu hunufaika isivyo halali kwa kufanya udanganyifu katika vipimo.
Kutokana
na hali hiyo, Serikali ilianzisha Bodi ya Mazao Mchanganyiko ili
kujikita katika biashara ya mazao ya nafaka na mengine yasiyo na chombo
cha usimamizi ili kumpa unafuu wa maisha mkulima.
Akiwasilisha
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19, Waziri wa
Kilimo Dkt. Charles Tizeba anasema kutokana na usimamizi imara wa
Serikali kupitia Bodi za mazao, uzalishaji wa mazao mbalimbali
umeendelea kuimarika hususani mazao ya asili ya biashara.
Anasema
kuwa katika mwaka 2017/18 Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko imenunua
tani 2,504.09 za mahindi kutoka kwa wakulima wa mikoa ya Iringa na
Ruvuma yenye thamani ya Tsh Bilioni 1.25.
Dkt.
Tizeba anasema hadi kufikia mwezi Desemba mwaka hadi kufikia mwezi
Desemba 2017 Bodi imesagisha tani 146.5 ambapo zimepatikana tani 112.7
za unga wa mahindi na tani 33.8 za pumba, ambapo usagishaji unaendelea
na mauzo yanaendelea katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Dar es Salaam na
Mwanza.
Anaongeza
kuwa katika kuongeza uwezo, Bodi imepokea mkopo wa Tsh Bil 3.66 kutoka
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kununua mashine yenye
uwezo wa kusagisha tani 60 za mahindi kwa siku na mashine yenye uwezo wa
kukamua tani 20 za mbegu za alizeti kwa siku zitakazofungwa katika eneo
la Kizota mjini Dodoma.
“Aidha,
Mashine hizo zitakapoanza kufanya kazi Bodi itaweza kununua tani 17,000
za mahindi na tani 6,000 za mbegu za alizeti kutoka kwa wakulima kwa
mwaka na mzabuni wa kufunga mashine hizo kampuni ya UGUR ya Uturuki
inatarajia kukamilisha ufungaji wa mashine kabla mwezi Julai, 2018”
anasema Waziri Tizeba.
Dkt.
Tizeba anasema katika mwaka 2018/19 Serikali itaendelea na uhamasishaji
wa uanzishwaji wa kilimo cha mkataba na kibishara kwa zao la muhogo
katika kanda za Mashariki na Kusini kwa kushirikisha Halmashauri za
Wilaya ya Mikoa ya Lindi, Mtwara, Manyara, Singida na Morogoro.
Kwa
mujibu wa Dkt. Tizeba anasema kilimo cha mkataba, Serikali itahamasisha
wakulima kulinda mazao ya mikunde, bustani na mafuta kibiashara kwa
ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.
Ununuzi
wa mazao ya wakulima kupitia Bodi ya Mazao utasaidia kuokoa uharibifu
wa mazao mengi ya nafaka yanayokaridiwa kabla ya kuvunwa yakiwa shamba
kutokana na tekonojia duni ya utunzaji na uhifadhi.
Kuandaliwa
kwa mfumo wa ukusanyaji wa takwimu za mazao ya chakula na mazao
yanayosindikwa viwandani, utasaidia kubaini wa mazao hayo upotevu katika
mnyororo wa thamani na kutengeneza mikakati ya kuboresha viwanda, na
hatimaye kutengeneza ajira na kipato.

No comments:
Post a Comment