Thursday, October 18, 2018

DKT ANGELINE MABULA AIWAKILISHA NCHI MKUTANO WA USIMAMIZI WA NYUMBA NA MIPANGO MIJI.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula ameiwakilishi nchi katika mkutano wa mawaziri wa bara la Afrika wanaosimamia sekta ya nyumba na maendeleo ya  mji uliofanyika katika nchi ya Senegal.

Aidha katika mkutano huo Mhe Dkt Angeline Mabula alipata wasaa wa kuwasilisha taarifa ya hali halisi ya nchi katika suala zima la utawala wa miji na usalama wake.

Katika hatua nyengine nchi ya Tanzania ilipata tuzo ya ushiriki wa mkutano huo iliyopokelewa na Naibu Waziri Mhe Dkt Angeline Mabula.






No comments:

Post a Comment