Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameagiza kurejeshwa ndani ya miezi
mitatu madeni yote yaliyokopwa kwenye vyama vya akiba na mikopo
(SACCOS).
Alisema
kuwa mwananchi watakaoshindwa kutii maelekezo hayo katika kukamilisha
deni lake ndani ya miezi mitatu hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao.
“
Nataka kila aliyekopa kwenye Saccos arejeshe deni lake kwa kufuata
utaratibu wa makubaliano na kama wasipotekeleza ndani ya miezi mitatu
niliyotoa serikali itaagiza wahusika wote kukamatwa maana dawa ya deni
ni kulipa” Alisisitiza
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa agizo hilo tarehe 14 Disemba 2018
wakati wa kikao cha kazi katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
alipokuwa akizungumza na viongozi wakuu wa vyama vya Akiba na Mikopo
(SACCOS) sambamba na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopo katika Mkoa
wa Mtwara.
Kikao
hicho kimehudhuriwa pia na Kaimu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini,
Mkaguzi wa vyama vya ushirika na Saccos, Kaimu Mrajisi msaidizi wa mkoa
wa Mtwara, Wenyeviti na watendaji wa SACCOS pamoja na vyama vya msingi
vya ushirika vilivyopo mkoani Mtwara.
Mhe
Hasunga amelitaka Shirika la Ukaguzi wa Hesabu za Vyama vya Ushirika
(COASCO) kutimiza majukumu yake kwa weledi kwa kukagua na kuhakikisha
vyama vyote vinafunga mahesabu huku akitaka vyama ambavyo sio hai
kuchukuliwa hatua.
Pia
ameagiza kila chama Tanzania kiwe na daftari la wanachama walio hai na
wafu sambamba na kuhakikisha kuwa viongozi wote wawe na maadili na uwezo
wa kuvisimamia vyama vyao ipasavyo.
Katika
hatua nyingine alimtaka Mrajis wa ushirika Tanzania Bw Tito Haule
kuwasilisha mpango kazi wa namna ya kukutana na wanachama wa ushirika
nchi nzima katika kutatua changamoto zao. “ Na ni lazima taarifa
itengenezwe ikionyesha idadi ya vyama mlivyokutana navyo na kueleza ni
mambo gani mmezungumza kila mwezi” Alisema
Aliongeza
kuwa Viongozi ni lazima kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya
Ushirika itakayosaidia kuondoa usumbufu kwenye ushirika ili uendelee
kuwa mkombozi wa wananchi. “Mje na mfumo wa namna ya kuwasaidia wananchi
kupata pembejeo bila kuingia madeni yasiyokuwa na tija” Alisisitiza
No comments:
Post a Comment