Na Yusuph LudimoMbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amewahakikishia ushirikiano wadau wa maendeleo ili kuhakikisha wananchi wa jimbo lake wanajikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa kwa niaba yake na katibu wa Ofisi ya mbunge, Ndugu Kazungu wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji kilichojengwa na Taasisi ya Tanzania Transformation Trust katika mtaa wa Masemele Toroto kata Bugogwa inayojishughulisha na kueneza neno la Mungu nchini mara baada ya kupokea ombi la mbunge huyo la kuwaomba kushirikiana nae katika kumaliza kero zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo, Hivyo kuamua kujenga kisima Cha maji Safi na mbunge kutoa tofali zote za Ujenzi wa kisima hicho.
'.. Niwahakikishie kuwa tutaendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuwaletea wananchi hawa maendeleo na waweze kujikwamu kiuchumi, Lakini si tu utekelezaji wa miradi Kama hii hata shughuli za uwekezaji tunaweza kuzifanya kwa pamoja na sisi tupo teyari ..' Alisema
Kwa upande wake muwakilishi wa Taasisi ya Tanzania Transformation Trust inayofanya kazi ya kueneza neno la Mungu kupitia Kanisa la Kristo Ndugu Erick Shiganga amesema kuwa Kanisa hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo pamoja na kutangaza neno la Mungu ili kuimarisha umoja, upendo, amani na mshikamano, Kama Mungu anavyotaka katika jamii zetu.
Aidha Diwani wa kata ya Bugogwa kilipojengwa kisima hicho, Mhe William Mashamba amemshukuru mbunge wa Jimbo hilo kwa namna anavyojitoa na kutafuta wadau ili kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Wananchi Mariana William na Deus Kanyerema wa Kijiji Cha Masemele Toroto walitoa ushuhuda wa namna wanavyopata adha na tabu ya maji kwa kuyafuata mbali na yakiwa si Safi na salama katika hadhara hiyo ya makabidhiano.
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya mbunge
Jimbo la Ilemela
01.06.2019











No comments:
Post a Comment