Mhe Stanslaus Mabula amesema hayo katika kata ya Mandu,
kisiwani kwenye ziara yake kata hiyo ambao ni mwendelezo Wa kutembelea
kata zote za halmashauli ya Jiji la Mwanza ili kuelezea utekelezaji Wa
Ilani ya uchaguzi, kusikiliza na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo
wananchi Wa jimbo la Nyamagana.
Mhe Mabula amewaambia wajasirimali wa Lishe zipo fedha
halmashauri ya Jiji Mwanza yeye pamoja na baraza la madiwani ni jukumu
lao kusimamia tengo la asilimia 10% mapato ya halmashauli kuwajengea
uwezo Wa kimtaji 5% Vijana na 5% wanawake.
Amefafanua kuwa serikali IPO katika mchakato Wa mwisho
kuwezesha vitambulisho vinapatikana kwa wajasirimali Wote ila ni vyema
pia kujiunga katika vikundi vilivyosajiliwa ili I we rahisi kunufaika na
taasis za kifedha katika kuboresha na kukuza biashara yao.
Wajasirimali hao 10 maarufu katika uchomaji Wa mihogo na
uuzaji wa kawaha pamoja na chai wamekuwa wakitumia mitaji yao
kujiengesha pasipo msaada Wa taasis za kifedha.
Wote kwa pamoja wamemuhakikishia mbunge kutumia fursa hiyo
kuanzisha kikundi na kukisajili. Naye mbunge amewaahidi ofisi yake
kuwapatia mtaalamu Wa andiko la katiba na la kibiashara pamoja na
kuwapatia elimu ya ujasirimali kisha kusimamia waweze kunufaika na tengo
la halmashauri kwa wajasirimali ambalo ni haki yao kwa mujibu Wa
Sheria.
Kadharika mhe mbunge akitumia fursa hiyo kununua mihogo hiyo na kushiriki pamoja nao chakula.
Imetolewa na:-
Of isi ya mbunge
Jimbo la Nyamagana
Of isi ya mbunge
Jimbo la Nyamagana
No comments:
Post a Comment