#"UVCCM tunawataka wabunge vijana kujipanga kimkakati,
kujibu hoja kwa nguvu ya hoja toka upinzani wenye lengo la kuishambulia
serikali au kumvunjia heshima Spika wa Bunge" Shaka
#"Tunawataka wakukutane haraka kutafakari na kujiweka
tayari kwani upinzani unataka kuligeuza Bunge kuwa ni uwanja wa
malumbano ya siasa kinyume na maudhui yake." Shaka
#"Kabla ya tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida
Mashariki, kulikuwa na mashambulizi hatari huko Kibiti, ikafuatia
kutekwa watoto Mkoani Arusha hatimaye Brigedia Jenerali wa JWTZ Visent
Masawe naye akapigwa risasi hadharani" Shaka.
#"Kumekuwa na hali ya kushangaza huku baadhi ya wanasiasa
wa upinzani kulishupalia mno tukio la Lissu na kutumia mwanya wa tukio
hilo ili kujipatia umaaarufu wa kisiasa.
#"Ukitazama tukio la Lisu linavyozungumzwa ni tofauti na
ilivyokuwa kwa matukio mfululizo ya mauaji ya Kibiti yaliovyopewa uzito
mwepesi. Nafikiri kuna jambo linapikwa ambalo watanzania wanapaswa
kugutuka na kung'amua mapema" Shaka
#"Viongozi na wabunge upinzani kimuonekano na kimatamshi
hawaonyeshi kuchukizwa kama wananchi wote wanavyoonekana kukerwa na
matukio ya kibiti, watoto kutekwa, kupigwa risasi Lissu na la Brigedia
Jenerali wa JWTZ" Shaka
#"Tumetafakari na kujiuliza kuna nini nyuma ya mkakati
huu, je mauaji ya kibiti, watoto kutekwa, kupigwa risasi Brigedia
yote si matukio mabaya yanayofanana na kama lile la Lissu, vipi basi
hili moja lipewe kipaumbele kwa kiasi hiki " Shaka
#"Napata mshango mkubwa kuonana kunaibuka hoja na
mijadala bungeni huku wabunge wa upinzani wakijaribu kutaka kuutikisa
mhimili mmoja wa dola na kukidharau kiti cha Spika" Shaka
#"Spika ni kiongozi wa juu nchini anayeongoza moja kati
ya mihimili mitatu ya Dola na kusema Bunge lina nidhamu, heshima na
umuhimu unaostahili kuheshimiwa na kila mbunge kulingana na uzito ule
ule" Shaka
#"Zipo dalili na maandalizi ya wabunge wa upinzani
kumsakama kwa maneno na tuhuma za kitoto Spika, lengo lao ni kuligeuza
Bunge liwe uwanja wa siasa na malumbano jambo hilo lisikubaliwe " Shaka
#"UVCCM hatupendelei kuliona bunge likiwa chombo cha
kuwakilisha wananchi, likiondoshewa haiba na majukumu ya msingi badala
yake lijiingize katika misokotano na mabishano" Shaka
#"Tutawashauri wabunge vijana wa CCM waandae mkakati
kabambe wa kupinga, kujibu na kuzima uzushi kwa nguvu ya hoja dhidi ya
utovu wowote wa nidhamu atakaofanyiwa Spika, Naibu Spika au wenyeviti
wa bunge katika vikao vyao " Shaka
#"Upinzani baada ya kuona kasi ya utendaji wa Serikali ya
Dk Magufuli ukipata mafanikio katika kusimamia mapambano ya rushwa,
ufisadi, mkakati wa kujenga uchumi, kuhimiza uwajibikaji na nidhamu ya
kazi, sasa wabunge wake wanaleta chokochoko" Shaka
#"Wabunge wa upinzani ni watunzi mahiri wa uongo, husema
mambo yakufikirika na yasiosadikika kusudio ni kujaribu kuikwamisha
Serikali, mpango wao kuligeuza bunge liwe eneo la uzushi na uongo kitu
hicho ni batili na haikubaliki" Shaka
#"Nawapongeza kwa kuchaguliwa kwenu vijana nendeni mkalinde chama cha Mapinduzi kwa uzalendo na uthubutu" Shaka
#"Tumuunge mkono Rais wetu Dk John Pombe Magufuli Vita hii
ya Uchumi ni kubwa na nzito Rais Magufuli ameonyesha nia na dhamira ya
kulinda na kutetea rasilimali za watanzania" Shaka
#"Vijana lindeni chama kwa kukitetea na kukipigani mkiongozwa na uthubutu na uzalendo" Shaka
#"Jeshi hili la vijana wa CCM lina dhamana kubwa ya
kuhakikisha makosa tuliyofanya mwaka 2015 mkoa wa DSM hayajirejei teba
naamini litafanya kazi nzuri na hatimae kuleta heshima ya kurudisha
majimbo na kata za mkoa wa DSM zilioko upizani' Shaka.
No comments:
Post a Comment