"Kinadharia na kiuhalisia Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa
kashfa ya Richmond Edward Lowassa yuko katika majuto makubwa kwa
kupitisha uamuzi wa kuhama CCM kutokana na hali ya kisiasa aliyoikuta
Chadema kuwa kinyume na matarajio yake" - Shaka
"Watu aliowashawishi kuondoka CCM na waliobaki amewakosesha
heshima na amana ya kisiasa aidha kwa walichohamia uongozini na wale
waliobaki CCM" - Shaka
"Jambo la kusikitisha kumuona Waziri Mkuu huyo wa zamani
akiwataka wanachama waliopo CCM waliokuwa wakigombea nafasi mbali mbali
na kutopitishwa na vikao kujiunga na Chadema wakati yeye mwenyewe yuko
mguu ndani mguu nje" - Shaka
"Lowasaa kimsingi amepoteza mvuto na heshima kisiasa
aliyokuwanayo kabla ya kuhama CCM na sasa amebaki ni Mwanasiasa
zilipendwa akijikongoja ili aonekane yupo wakati ameshachujuka." -
Shaka
"Lowassa asiudanganye ulimwengu kama bado angali na mvuto
wa kisiasa kama alivyokuwa CCM iliyompa heshima, umaarufu na kuheshimika
kisiasa. Amehama na sasa amebaki kama Samaki aliyetolewa nje ya maji" -
Shaka
"Hakuna Mwana CCM yeyote anayetengwa, anayebughiwa au watu
kumnyanyapaa kama anavyodai Lowassa kwa lengo la kutaka kujitutumua
kisiasa na aonekane yupo yupo." - Shaka
CCM inafuraha kubwa kumuona Lowassa akikubali kuuungana na
wale waliomtukana, kumwita fisadi, mwizi na mbadhirifu wa mali za umma
sasa akiwafanya marafiki. Itakuaje Mtu akutukane mchana kisha usiku
akusifu, na wewe uone fahari, ajabu!" - Shaka
"Lowassa ameshiriki kutenda kosa la kihistoria katika siasa
kwa kukubali kukiacha chama alichokitumikia muda mrefu na kujiunga
Chadema huku akimrubuni Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ng'ombale
Mwiru naye amfuate na kumpoteza kwenye ramani ya kisiasa." - Shaka
"Wana CCM msibabaishwe kabisa na maneno ya Wanasiasa wa
upizani ambao kwa sasa nidhahiri wanaonekana kutapatatapa na kutaka
kujitutumua ili waje juu wakati amemalizika na kufilisika kisiasa." -
Shaka
"Wananchi wote wanajua yaliofanywa na kundi la Mafisadi
kuiibia nchi rasiliamli za Taifa, kuingia mikataba ya hovyo, kupora
mashamba na Ranchi za Taifa huku wakifahamu uchumi wa nchi ni kina nani
waliouvuruga na kutufiksha hapa tulipo" - Shaka
"Hakuna Mwanasiasa yeyote mwenye jeuri na ubavu wa kuhama
CCM hata leo na kudhania anaweza kuwa na matarajio ya kuendelea kupata
umaarufu na heshima ya kisiasa kama alivyokuwa wakati akiwa chama
tawala." - Shaka
"CCM ni chama kikubwa chenye uzoefu mkubwa katika masuala
ya siasa, utawala na diplomasia hivyo haiwezi hata siku moja kutishika
kwa kivuli cha Lowassa, Kingunge au Fredrick Sumaye." - Shaka
"Nguvu za Mamba ni pale anapokuwa ndani ya maji ya mto au
ziwani, ukimweka nchi kavu anaweza kupigwa mieleka hata na fisi na
wala asifurukute au kujitetea kwa lolote. Lowassa anajitisha kwa kivuli
chake" - Shaka
Shaka H. Shaka ni Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa
No comments:
Post a Comment