Na Mwandish wetu Florah
Mhe Stanslaus Mabula amepokea benchi 20 zenye thamani ya
shilingi million 3 kutoka Shirika la BIMA ya taifa (NIC) za kupumzikia
wagonjwa au watu wanaoenda kupata huduma ya afya katika hospital ya
Wilaya Butimba.
Mkurugenzi wa BIMA ya afya ndg Samu Kamanga amekabidhi
bench hizo kwa mbunge wa Nyamagana na kwa mgeni rasmi mkuu wa Wilaya wa
Nyamaga mhe Mary Tesha mapema Leo. Mhe Kamanga amesema taasis yake
imetoa msaada kutoka ombi la ofisi ya mbunge Wa Nyamagana ili kusaidia
mandhari Rafiki na salama kwa watu wanaofika eneo hilo ili kupata
huduma. " Taasis yangu itaendelea kushirikiana na ofisi hiyo katika
maeneo mengine yenye uhitaji Wa haraka." Alisema.
Mgeni rasmi mkuu Wa wilaya Ndg Mary Tesha amepongeza taasis
hiyo ya BIMA kwa kushiriki shughuli za kijamii na kuwaomba wasiachie
hapo waangalie na maeneo mengine ikiwa ni vifaa tiba na vifaa vya
hospital.
Naye mbunge jimbo la Nyamagana ameshukuru kwa msaada huo
uliotolewa kwa uharaka na wepesi. Nakuhaidi ofis yake ipo tayari kutoa
ushirikiano na taasis hiyo katika kukabili changamoto za wananchi Wa
jimbo la Nyamagana.
Hafla hii ya makabidhiano imefanyika hospitalini hapo na
kuhudhuliwa na mkuu wa wilaya Nyamagana ndg Mary Tesha, kaimu mkurugenzi
wa halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg, Kusiga na mganga mkuu wa Jiji Dkt
Edru pamoja ya viongozi wa hospital ya Butimba.
Imotelewa:-
Ofisi ya Mbunge,
Jimbo Nyamagana.
Ofisi ya Mbunge,
Jimbo Nyamagana.
No comments:
Post a Comment