Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein
akimuapisha Aziza Iddi Suwedi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar
katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi
wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimuapisha George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya RaisKatiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, kabla alikuwa Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar.
Baadhi ya Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar walioapishwa leo na Viongozi wengine kazi iliyofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya kuwaapisha rasmi leo katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment