Monday, October 2, 2017

VIJANA WAASWA KUJIUNGA NA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI ILI KUKIKWAMUA KIUCHUMI NA KUCHAGIA PATO LA TAIFA.

Vijana waaswa kujiunga na vikundi vya uzalishaji Mali ili kujikwamua kiuchumi na kuchagia pato la taifa.
Maneno hayo yamesemwa na mbunge jimbo la Nyamagana mheshimiwa Stanslaus Mabula kwenye ziara kata ya Buhongwa alipokutana na kundi la Vijana waendesha boda boda, wauza kahawa na mama lishe katika mwendelezo wake Wa ziara yake katika kata zote 18 za halmashauri ya Jiji la Mwanza kukagua miradi ya Maendeleo, kukutana na makundi maalum na wananchi ili kusikiliza kero zao na kuweza kuzitatua.
Mhe Mabula amewapongeza Vijana kushiriki shughuli za uzalishaji Mali na kuwahamasisha kujiunga na vikundi vya wajasirimali kwa shughuli zinazoshabihana ili waweze kunufaika na 10% ya mapato ya halmashauri ya Jiji la Mwanza ambalo ni takwa Ki Sheria.
Mapato ya Jiji yanapatikana Kwa kodi ya wana Nyamagana, na Mimi kama mwakilishi wenu nitahakikisha na shirikiana na balaza la madiwani kuisimamia halmshauri yetu iweze kutoa 5% kwa vijana na 5% kwa wanawake iwajengee uwezo Wa kimtaji kwa mikopo ya riba nafuu. Alisema
Wauza kahawa wa kata hiyo wamemhakikishia mbunge utayari wa kuanzisha vikundi vya wauza kahawa ili kunufaika na 10% ya mapato ya jiji. Na kuomba usaidizi Wa ofisi isaidie fedha hizo ziwafikie walengwa hususani Wa biashara ya kahawa ambao mtaji wao sio Mkubwa ni 100,000 kwa kila mmoja.
Ziara hii mhe mbunge ameambatana na mwenezi Wa Kata ya Buhongwa Ndg Hassan Bushagama, mwenyekiti wa mtaa Bulale Ndg Regina Vigeyo. Mwenyekiti wa CCM Bulale Ndg Shija Mahenge. Mwenyekiti wa mtaa wa Nyangwi Ndg, Zabron Ngese.
Imetolewa na:-
Ofisi ya Mbunge,
Jimbo la Nyamagana.




No comments:

Post a Comment