"Taasisi
mbalimbali za umma na zisizo za umma zinazomualika Rais katika shughuli
zao zinakumbushwa kutokutangaza ushiriki wa Rais katika shughuli zao
mpaka zipate uthibitisho kutoka ofisi ya Rais", imesema taarifa
iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Jijini Dar es
Salaam, leo.
Taarifa
hiyo imesema, inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli hatakuwa mgeni rasmi
katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama
inavyotangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Tarehe
11 Oktoba, 2017 ambayo inatangazwa kuwa ndio siku ya kufanyika kwa
kongamano hilo, Rais atakuwa na majukumu mengine ya Kitaifa kulingana na
ratiba yake ya kazi.
No comments:
Post a Comment