Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli amefurahishwa na kazi inayofanyika ya kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa wa Mwanza ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Viwanda vinavyochukua watu wengi na kupunguza tatizo la ajira nchini
Mhe Dkt John Magufuli ameyasema hayo leo akiwa katika viwanja vya Mwatex wilayani Ilemela alipohutubia wananchi wa mkoa huo kupitia ziara yake ya siku mbili mkoani humo mara baada ya kufungua daraja la watembea kwa miguu la Furahisha na uzinduzi wa kiwanda cha Sayona vyote vikijengwa ndani ya wilaya ya Ilemela ambapo ameambata na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwigaje, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula, Mbunge wa Vijana Mhe Maria Kangoye, Wakuu wa Wilaya, na Wakurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu John Wanga na Jiji la Mwanza Ndugu Kiomoi Kibamba
Mheshimiwa Mkuu wa mkoa niseme tu kwa hili la ujenzi wa viwanja nakupongeza sana sana, na nitoe rai kwa wakuu wengine wa mikoa kujifunza na kuanza kujenga viwanda kwenye maeneo yao Alisema
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kumshukuru Mhe Rais Magufuli ametaja miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Jimbo lake ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya Karume, miradi mikubwa ya maji na ujenzi wa barabara za Buswelu, Kiseke na Airport
Akihitimisha Mkuu wa mkoa Mwanza Mhe John Mongela mbali na kumshukuru Mhe Rais kwa ziara yake ameyahakikishia ushirikiano makundi mbalimbali ya kijamii katika kujiletea maendeleo na ujenzi wa nchi ya viwanda yenye uchumi imara .
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
30.10.2017




No comments:
Post a Comment