Ndugu zangu nasema leo nina furaha kama jina la daraja kwa sababu mimi
natambua historia ya eneo hili. Eneo hili lilikuwa linatambulika kama
blackspot kwa sababu ya ajali nyingi sana kutokea hapa
Nakumbuka wakati naomba kura nilisema nitatengeneza daraja la Furahisha.
Wananchi mkasema haiwezekani, nikasema itawezekana. Nashukuru wananchi
wa Mwanza ka kutuamini
Wananchi sisi wote kama madiwani na wabunge na mimi kama kiobgozi wenu tutafanya kazi kweli kweli na kuijenga Mwanza
Nilivyokuwa waziri wa ujenzi kwa kushirikiana na Mkuu wa mkoa tulifunja
nyumba ili kutanua barabara, leo naona mmevunja nyumba ya Madaraka.
hongereni sana maana ilikuwa sehemu ya wazi. Pia hongereni kwa kuvunja
nyumba ya CCM amabayo ilikuwa kwenye sehemu ya road reserve. Na mimi
nilijivunjia ukuta wa nyumba yangu pale Solomoni Nassor. Wakaandika
waziri ajivunjia ukuta
Nilipozuia sherehe za Mapinduzi watu walisema sipendi hata mapinduzi
lakini nikasema mimi ni rais na nimeamua kutuma fedha hizo kutengeneza
Mwanza na zile za uhuru zilijenga Dar es Salaam. Inaweza tokea sherehe
nyingine nikasema fedha hizo zikajenge sehemu nyingine
Sidhani kama kuna daraja kama hili sehemu yoyote ya Tanzania, daraja
linajiwasha tu taa lenyewe na ndugu zangu wa Mwanza mtafungia ndoa hapo
Ndugu zangu naomba mlitunze daraja hili, kwanza linaonyesha picha ya samaki hata aliyetengeneza daraja hili anakula samaki
Mwanza ya miaka ya nyuma si miaka hii mwanza inabadilika, mimi na
viongozi wenzangu tunataka kuibadilisha mwanza, ndio maana tumetanua
barabara hii. Kwa sasa kunakazi ya kutanua uwanja wa Mwanza, ndege zote
za International nataka zitue Mwanza.
Leo nimeambiwa kuwa kandarasi alikuwa anashida ya fedha kidogo bilioni
9. Mwaziri mwambie mkandarasa atapata fedha yake wiki hii na nataka
uwanja huo ukamilike ndani ya muda wangu kuisha. Usipo malizika yeye
ndio atamalizika hapo hapo
Mbali ya kuendeleza sekta ya usafirishaji wana Mwanza mnafahamu kuwa
tunajenga reli ya standard Gauge inayotoka Dar kuja Mwanza itaenda
Rwanda mpaka Burundi Mpaka kigoma. Tunaijenga kwa fedha zetu bila
kukopa.
Kwenye Ziwa Victoria tutanunua meli kubwa itakayochukua watu zaidi ya
1200 na tani nyingi zaidi. Tutafanya ukarabati wa meli za Mv. Victoria
ili kuondoa shida ya usafiri
Tunafanya pia ukarabati wa meli nyingine kule Kigoma [Mv. Lyemba] ili
zirudi katika hali yake mpya. Tukiwa na Meli hapa itakuwa inaenda Bukoba
hadi Musoma
Tumeanza mikakati ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami, barabara
toka Usagara kwenda Kisesa imekamilika kwa asilimia 80% kwa kiwango cha
lami.
Daraja la Busisi hadi Kigogo usanifu umeshaanza, utengenezaji
unawezekana. Kila kitu kipya huwa ni miujiza hata niliposema mtu anaweza
kutoka Mtwara mpaka Mwanza kwa kutumia lami watu walidhani nimuujiza
ila leo imewezekana
Palikuwa na Mabango pale wasidhani sijayasoma nimeyasoma, kuna moja
lilikuwa linahusu watu walijenga eneo Kidoto na Muhonze wameambiwa
wamevamia eneo la uwanja wa ndege na eneo la jeshi. Hivyo wameambiwa
waondoke. Hili mimi natakiwa nilifanyie uchambuzi kwanza. Niwaombe
viongozi wasiwabomboleshe kwanza hawa watu mpaka nitakapotoa neno.
Hawa watu wa Kidoto na Muhonze ndio wamenipa urais na kwa vile serikali
yangu ina huruma na kwa mujibu wa sheria namba 4 ya mwaka 1999 na ya
vijiji namba 5 ya mwaka 1999 na kwa mijibu wa sheria ya mipango miji na
matumizi bora ya ardhi ya mwaka 2007 ardhi zote msimamizi wake ni rais
nasema wasiwabomoleshe kwanza. Waziri wa ardhi na viongozi wa chama
(CCM) na wakuu wa mikoa mkae wiki ijayo mtoe mapendekezo. Yapo maeneo
ambayo lazima watu wahame kama wale amabo wapo ndani ya airport.
Niwaombe watu wa Mwanza mlinde daraja hili msipitishe pikipiki pale. Pia litatumika kama Kivutio sio lazima muende airport
Huku akimuita mbunge fulani wa CUF aliyepo hapa. Huyu ni mbunge wa CUF
anatoka Lindi, naomba nimpongeze sana. Hizi ndivyo siasa za tanzania
zinatakiwa ziwe. Sehemu ya kupongeza pongeza sio unapinga tu huo unakuwa
ni uzito wa mawazo fulani kichwani. Hata sisi tunawapongeza CUF kwa
mambo ya maendeleo mfanyabiashara.
Rais Magufuli amesha zindua daraja hili kwa kukata utepe na ameondoka
eneo hili ka Furahisha. Rais magufuli anaenda kuzindua kiwanda cha
Mwatex kilichopo Nyakat.

No comments:
Post a Comment