Tuesday, November 21, 2017
ALIYOYASEMA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI KATIKA KIKAO NA WANAHABARI.
Tarehe 21/11/2017.
1. "Leo Chama kimepokea watanzania wenzetu ambao wameguswa na mageuzi makubwa tunayoyafanya." Humphrey Polepole
2. "Wanachama waliomba kurudi ni wanachama 200, wapo wabunge, wenyeviti wa kanda, viongozi na watendaji wa upinzani." Humphrey Polepole.
3. "Vitendo vyovyote vya ubadhilifu wa mali za umma ama za Chama havitavumiliwa na Chama ama na serikali ya Awamu ya Tano." Humphrey Polepole.
4. "Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa wametafakari wamejadili wameridhia Ndg. Sophia Simba kurudi ndani ya CCM." Humphrey Polepole.
5. "Tunamtaka Ndg. Sophia simba awe sehemu ya mfano bora kwa wanachama wengine." Humphrey Polepole.
6. "Chama kimefanya uteuzi wa wagombea wenye vigezo na waliomba dhamana ni 3004 na nafasi zilizopo ni 201." Humphrey Polepole.
7."Wenye Makando kando wote hawakupitishwa na vikao." Humphrey Polepole.
8. "Wale ambao hawakupitishwa na hawana makando kando Mwenyekiti ameagiza waendelee kuwa wanachama wema."
Humphrey Polepole.
9. "Mkoa wa Magharibi watarudia tena kupata wagombea wa Uwenyekiti wa mkoa, walioomba hawajakidhi vigezo vya CCM Mpya." Humphrey Polepole
10. "Ukisoma Kanuni yetu fungu la 22,
Mwanachama anayeomba nafasi ya uongozi ya utendaji hata ruhusiwa kushika nafasi nyingine ya aina hiyo ndani ya chama, Mtu mmoja kofia moja." Humphrey Polepole.
11. "Halmashauri Kuu inakitu kinaitwa Kapu, na kipindi hik walipatikana wanachama 531, na wanatakiwa watu 30."
Humphrey Polepole.
12. "Nafasi 15 kundi la Tanzania Bara tumependekeza watu 50." Humphrey Polepole
13. "Walikuwepo watu wameomba nafasi madiwani, wabunge kanuni imewakataa. Na majina yao hayajarudi na kikao kimekubali." Humphrey Polepole
14. "Kitu ambacho ni chama maana kabisa ni uanachama wa imani."
Humphrey Polepole
15. "Kama upo humu na unanafasi nyingine uwe kwenye Chama ama kwenye serikali ukichaguliwa tunakufuta nafasi hiyo." Humphrey Polepole
16. "Nyumba ya CCM, ni nyumba kubwa mchakato huu uwe nikipimo cha ustahamilivu, uvumilivu kwa wanachama." Humphrey Polepole
Imeandaliwa na kutolewa:
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI.
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment