Wednesday, January 24, 2018

KATIBU WA VIJANA ILEMELA ATEKELEZA AGIZO LA MWENYEKITI UVCCM TAIFA

Mwandishi Yusuph Ludimo
Katibu wa Jumuiya ya Umoja  wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela Comred Nehemia Philemon ametekeleza agizo la Mwenyekiti wa UVCCM Taifa la kuwataka makatibu wote wa jumuiya hiyo nchini kuonana na maafisa maendeleo wa manispaa zao  kuhakikisha asilimia Tano kwa vijana na Wakina mama  zinatengwa na kuwafikia  wahusika.

Akiwa manispaa ya Ilemela mara baada ya kikao chake na Afisa Vijana wa wilaya hiyo,  Comred Nehemeia Philemon  amesema kuwa manispaa yake anayoisimamia  imekuwa ikifanya vizuri katika zoezi la utengaji wa asilimia Tano za vijana na wakinamama  hivyo utekelezaji wa agizo alilolitoa Mwenyekiti UVCCM Taifa  Ndugu Kheri James walishaanza kulifanyia kazi  muda mrefu na  kinachofanyika sasa ni muendelezo kwa kuhakikisha wanaongeza usimamizi na ufuatiliaji ili fedha hizo zinazotoka ziweze kuwafikia vijana wengi huku akiwaomba vijana wanaonufaika na fedha hizo  kuwa waaminifu kwa kuzirejesha fedha hizo ili ziweze kusaidia na vijana wengine.

‘.. Nimefika hapa ili kuzungumza na wenzetu wa halmashauri ya manispaa Ilemela ili kuona zile asilimia tano wanazozitoa kwa makundi ya vijana na kina mama zinawezaje kuwafikia walio wengi  kama ambavyo mheshimiwa mwenyekiti wa jumuiya yetu ya vijana Kheri James ameelekeza, Pamoja na kwamba manispaa hii imekuwa ikitekeleza matakwa ya kisheria ya utengaji wa fedha hizo kwa muda mrefu sasa …’  Alisema.

Kwa upande wake Afisa Vijana wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Jumanne Maseke amemuhakikishia ushirikiano katibu huyo wa Vijana katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira bora na rafiki yatakayowasaidia vijana wa wilaya hiyo kwenda sambamba na Sera ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Maguli ya HAPA KAZI TU na kuwa na Uchumi wa Viwanda kwa kutoa elimu ya ujasiriamali, kutoa mikopo kwa vijana ambayo itasaidia katika kupunguza  changamoto ya ajira nchini kwa kutumika kama mitaji katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo wanazozifanya
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’.

Imetolewa na
Ofisi ya Umoja wa Vijana (UVCCM)
Wilaya ya Ilemela
24.01.2018





No comments:

Post a Comment