Mwadishi Yusuph Ludimo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi
Atashasta Nditie ametembelea Jimbo la Ilemela kujionea changamato za
mawasiliano zinazolikabili Jimbo hilo hasa maeneo ya Visiwani na nje ya
Mji kufuatia ombi la Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula
Akiwa Jimboni humo Mhe Mhandisi Nditie amefika kata za
Sangabuye na Kayenze na kujionea kero na changamoto ya kimtandao
inayowakabili wananchi wa maeneo hayo na kusababisha kukosekana kwa
mawasiliano ya uhakika kunakopelekea kukwama kwa shughuli za maendeleo
ambapo amewahakikishia wakazi wa maeneo hayo juu ya kutafuta ufumbuzi wa
kudumu kumaliza kabisa changamoto hiyo inayowakabili.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline
Mabula mbali na kumshukuru Naibu Waziri huyo kwa kutembelea Jimbo la
Ilemela ameongeza kuwa ziara aliyoifanya Naibu Waziri huyo ni matokeo
ya Ombi lake la kumtaka kuja kujionea hali halisi yachangamoto ya
kimawasiliano wanayoipata wananchi wake huku akiwataka wananchi na
viongozi kuendelea kushikamana na kushirikiana katika kufikia malengo
ya Serikali ya awamu ya Tano chini Mhe Rais Dkt John Magufuli
‘… Ziara hii ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano ni
matokeo ya ombi langu nililomuamba kufika katika Jimbo langu ili ajionee
changamoto na kero ya mawasiliano wanayoipata wananchi wangu hasa wa
pembezoni mwa mji na wale wanaoishi maeneo ya Visiwani kikiwemo kisiwa
cha Bezi ili na wao wakae waone wanaweza kutusaidiaje kumaliza
changamoto hii …’ Alisema Mhe Dkt Angeline.
Katika ziara hiyo Mhe Mhandisi Atashasta Nditie
aliambatana na wataalamu kutoka wizara yake na wataalamu kutoka Kampuni
ya Simu za Mkononi ya Halotel ambao wameahidi kujenga mnara wa Simu ili
kuhakikisha yanakuwepo mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wa maeneo
hayo.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa naOfisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
09.01.2018.






No comments:
Post a Comment