Mwandishi Yusuph Ludimo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula ameanza
ziara ya kutembelea Halmashauri kuu za Chama cha Mapinduzi kwa kata
zote 19 za Jimbo la Ilemela kueleza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
aliyokabidhiwa na chama chake mara baada ya kushinda kiti cha Ubunge
mwaka 2015.
Mhe Dkt Angeline Mabula leo ameanza kwa kuitembelea kata ya
Kayenze kabla ya kufika Sangabuye na baadae kuhitimisha kata ya Bugogwa
akiambatana na wataalamu wa Serikali kwa ngazi ya kata husika, madiwani
wa kata husika, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM, Katibu wa Umoja
wa Wanawake UWT na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa wilaya hiyo.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe Dkt Angeline Mabula ameeleza
juu ya shughuli na miradi mbalimbali ya Uvuvi na Kilimo, Elimu, Afya,
Maendeleo ya Jamii na Ustawi, Maji, Miundombinu na Ujenzi iliyotekelezwa
katika Jimbo lake kama inavyotaka Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake
huku akitaja baadhi ya vitu hivyo kuwa ni Uboreshaji wa Elimu na
Miundombinu yake kwa kugawa kompyuta kwa baadhi ya shule, kugawa
matofali kwaajili ya ujenzi wa madarasa na taasisi nyengine za Umma,
kugawa Madawati kwa shule za jimbo lake kupitia fedha za mfuko wa Jimbo,
mfuko wa The Angeline Foundation na wadau wengine, Kufungua barabara
mfu za mkoloni kupitia fedha za mfuko wa Jimbo na fedha binafsi,
kukarabati majengo ya baadhi ya Vituo vya afya kikiwemo Buzuruga,
kuwalipia wazee na watu wasiojiweza huduma ya Tiba kwa kadi TIKA,
Ujenzi wa madaraja na Ujenzi wa visima vya Maji safi na salama .
‘… Ndugu zangu mie ni muuza duka na wenye duka ni nyie
chama cha mapinduzi hivyo nimekuja kutoa hesabu za nilichokifanya tangu
mnikabidhi duka lenu, Yapo mambo mengi tumeyafanya baada ya kukabidhiwa
Ilani ya Uchaguzi na leo tumekuja kuwaeleza tuliyoyafanya kwa kipindi
cha miaka miwili tangu mtupe ridhaa hii …’ Alisema.
Aidha Mhe Dkt Angeline Mabula hakuacha kuelezea juu ya
umuhimu wa zoezi la urasimishaji na upimaji makazi na kuwataka
kuhakikisha wanapata hati miliki ya maeneo yao ili kuyaongezea thamani
na uhalali huku akiwachangia kiasi cha pesa wakazi wa kata ya Kayenze
walipomuomba kuwaunga mkono kufanikisha ujenzi wa shule yao ya Sekondari
ili kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo sanjari
na kuwaomba kutumia nishati ya umeme vijijini REA katika shughuli za
uzalishaji kupitia sera ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais
Dkt John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.
Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa wilaya hiyo
Komredi Dennis Lekela Kankono aliyewakilisha Uongozi wa Chama kwa
ngazi ya wilaya mbali na kukiri kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani
unaofanywa na Mbunge Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka madiwani na
wenyeviti wa mitaa kuiga mfano wa alichokifanya mbunge kwa kuhakikisha
wanatoa taarifa za utekelezaji wa Ilani kulingana na ngazi ya
halmashauri kuu zao kwa maana ya kata na matawi.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
11.01.2018
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
11.01.2018









No comments:
Post a Comment