Yusuph Ludimo anaripoti
Wananchi wa Jimbo la Ilemela wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika uchangiaji wa shughuli za maendeleo .
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt
Angeline Mabula wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu wa kata
za Shibula, Kahama na Buswelu kupitia ziara yake ya Jimbo kwa kata zote
za wilaya hiyo kueleza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama cha
mapinduzi aliyokabidhiwa mara baada ya kushinda ubunge ambapo amewaasa
kuhakikisha wanachangia shughuli za kimaendeleo ikiwemo uchangiaji wa
huduma za afya, miundombinu, maji, umeme na elimu huku akikumbusha
wajibu wa wazazi, kamati za shule na jamii katika suala zima la
kufanikisha elimu bila malipo.
‘… Ndugu zangu elimu bila malipo haiondoi wajibu wako kama
mzazi, haiondoi wajibu wako kama jamii hivyo ni lazima tuchangie
shughuli za maendeleo ili kusaidia watoto wetu tusiachie Serikali kila
kitu, Kila mmoja anawajibu wake, Kamati za shule zinawajibu wake na bodi
za shule zina wajibu wake …’ Alisisitiza.
Aidha Dkt Angeline Mabula amekemea tatizo la mimba za
utotoni , amefafanua juu ya umuhimu wa zoezi la urasimishaji makazi na
umilikishwaji wake pamoja na kumshukuru Mhe Rais Dkt John Magufuli kwa
sera ya Elimu Bure na msaada wa gari la kubebea wagonjwa alilolitoa kwa
hospitali ya Sangabuye Ilemela huku akiwataka wananchi kumuunga mkono
kwa kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali kupitia Ilani hiyo ya
Uchaguzi.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buswelu Mhe Sarah Ng’wani
amewataka wajumbe wa halmashauri kuu wa kata yake kuwa chachu katika
kuhamasisha shughuli za kimaendeleo na kuwa wavumilivu ili kuwapa
nafasi wawakilishi waliowachagua kutekeleza yale yaliyoelezwa katika
Ilani ya Uchaguzi.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya Shibula Ndugu
Amos Lungisa amewataka wananchi wa kata yake kutokatishwa tama
wanapojitoa kufanikisha shughuli za maendeleo sanjari kuwaunga mkono
viongozi wao waliowachagua.
Katika Ziara hiyo ya utekelezaji wa ilani aliambatana na
viongozi mb.alimbali wa chama cha mapinduzi na jumuiya zake zote kwa
ngazi ya wilaya na watendaji wa Serikali kwa kata zote zilizohusika
wakiongozwa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa wilaya hiyo.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa naOfisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
11.01.2018









No comments:
Post a Comment