Bweni la wasichana wa shule ya sekondari Kipoke mkoani Mbeya limeteketea
kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa huku wanafunzi wawili
wakijeruhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa shule hiyo Gervas Mwanyila wakati
alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari wa EATV na kusema ni kweli
tukio hilo limetokea katika shule yao japokuwa mpaka sasa hawajafahamu
chanzo chake.
"Ni bweni la wasichana kidato cha pili limeungua moto ambapo mpaka sasa
hatujajua chanzo chake kama ni umeme au ni wanafunzi wenyewe tumeshindwa
kufahamu. Tumefanya jitihada za kunusuru vitu vya wanafunzi na wao
wenyewe lakini tumefanikiwa kwa kiasi kidogo kutokana na baadhi ya vitu
ikiwemo magodoro na vitanda 68 kuteketea na moto", amesema Mwanyila.
Pamoja na hayo, Mwanyila ameendelea kwa kusema "ni vijana watano pekee
waliojeruhiwa kidogo na moto huo baada ya wao kusaidia kukata bati ili
moto usiweze kuenea katika maeneo mengine ya bweni".
Kwa upande mwingine, Mwanyila amesema bado hawajaweza kujuwa tathimini
kamili ya mali za shule zilizoweza kuteketea na moto kutokana bado
hawatulia tokea ajali hiyo ya moto ilipoanza.

No comments:
Post a Comment