Wednesday, February 14, 2018

CHADEMA HAWANA CHAO MWANZA: MWENYEKITI UVCCM TAIFA COMRADE KHERI D JAMES LEO TAREHE 14/2/2018 KATIKA MKUTANO WA KUMUNADI MGOMBEA UDIWANI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU NYAMASIRIRI KATIKA KATA YA ISAMILO (W)NYAMAGANA MKOA WA MWANZA


Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Taifa comrade Kheri D James na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi akihutubia mkutano wa kampeni uliohudhuliwa na mamia ya wakazi wa jiji la mwanza katika kata ya Isamilo mtaa wa NERA ,

Amewambia vyama vya upinzani hawana chao kwa sasa ndani ya mkoa wa mwanza na Tanzania kwa ujumla na waache kupoteza mda wa kutukana majukwaani  na kuwarubuni vijana kwa ahadi za uongo zisizotekelezeka.

Mwenyekiti aliendelea kuwambia wana mwanza wanaimani kubwa sana na ccm  ndio mana wabunge wengi ni wa ccm na hapa Nyamagana mbunge ni wa ccm ,Meya wa ccm madiwani asilimia tisini na tano (95%) ni wa CCM.

Maendeleo yanaletwa na serikari ya ccm chini ya mwenyekiti wa ccm Taifa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kipenzi cha  Watanzania 

Rais wetu kafanya mambo mengi na yenye tija kwa watanzania
Leo machinga wanajivuna sababu ya mbunge makini wa ccm Mhe S Mabula  na Rais Makini na  msikivu .

Elimu bure ccm,huduma za afya zimeboreshwa ccm,miundo mbinu safi na kwa sasa jiandaeni na Reli ya kutoka mwanza mpaka Dar kazi ya ccm chini ya Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli
Mwenyekiti alisema kazi ya chama chetu ni kutatua kero na changamoto zinazo wakabili wana mwanza na watanzania  wakati vyama vya upinzani kazi yao nikuwatukana viongozi hiyo ni dalili ya  kuonyesha wamefilisika kifikira na hawana tena CHAO.

Comrade kheri alimuomba waziri wa mambo ya ndani kuwa onya wanao sumbua wananchi kwa vitisho kabla hajatoa maelekezo kwa vijana wake (uvccm)

Waziri Mwiguru ambae na yeye alikuwa sehemu ya wageni waliohudhuria mkutano huo  alipata nafasi ya kuhutubia nakuwaondoa wasiwasi wakazi wa Isamilo (w)Nyamagana mkoa wa mwanza kwa kuwaondoa hofu juu ya mambo ya ulinzi na usalama .

Pia aliwasii wana Isamilo tarehe 17/2/2018 kumuchagua Diwani wa Ccm na wajitokeze kwa wingi .
Wageni wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mbunge wa jimbo la Ilemelela na naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi Mama A Mabula .

Mama Mabula aliwaondoa wasiwasi  wakazi wa mwanza kwa kuwaambia kaeni na amani nyumba zenu haziwezi bomolewa bila sababu za msingi .

#TUKUTANE KAZINI
NAJIVUNIA KUWA MWANA CCM
HUSSEIN A KIMU
KATIBU HAMASA NA CHIPKIZI MKOA WA MWANZA 





 

No comments:

Post a Comment