Mwandishi Hussein A. Kimu
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa Comrade Kheri D James leo tarehe 13/2/2018 katika kata ya kanyerere wilaya ya misungwi mkoa wa mwanza amewafunda mamia ya wananchi walio hudhuria katika mkutano wa hadhara wa kumunadi mgombea udiwani wa chama cha mapinduzi ndugu Daniel .
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa alianza kwa kufikisha salamu za Mhe Rais wa Jamuhuri ya muungano na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa Dr John Pombe Magufuli
Kwakuwambia Rais wetu anawapenda sana wana kanyerere wana misungwi na watanzania wote
Rais wetu mpendwa amejitoa kwa ajili ya watanzania wote wapenda maendeleo hasa wanyonge wote tuendelee kumuombea na kumuunga mkono .
Mwenyekiti aliwafunda wana misungwi kwa kueleza faida za kumuchagua mgombea anaetokana na chama cha mapinduzi
Pia mwenyekiti aliwaomba wananchi walio hudhuria mkutano huo kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi na serikari yake mana ndio wenye jukumu la kweli la kuleta mabadiliko yenye tija kwa watanzania
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa chama na jumuiya zake ngazi ya wilaya mkoa na wabunge akiwemo Mbunge wa Ji mbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula
TUKUTANE KAZINI



No comments:
Post a Comment