Maandamano makubwa yatarajiwa hii leo Nairobi kuishinikiza serikali
kuvifungua vyombo vitatu vya habari nchini vilivyofungiwa kupeperusha
matangazo kwa siku ya saba leo.
Maandamano haya yanajiri wakati viongozi wa upinzani waliokamatwa kwa
madai ya kushiriki njama ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga
kama rais.
Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa
madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja matangazo licha ya onyo
kutofanya hivo.
Na sasa makundi ya kutetea haki za kibinadamu, waandishi habari na
baadhi ya wananchi wanapanga kufanya maadamano hii leo Nairobi
kuishinikiza serikali kutii amri ya mahakama.
Waandalizi wa maandamano hayo wanaishtumu serikali wakidai imekiuka haki
za kibinadamu, kuendeleza mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari kando
na kupunguza uhuru wa demokrasia nchini kwa kutoheshimu katiba.
Kufutia kuapishwa kwa Odinga Jummanne iliyopita, vyomba vya usalama vime
wakamata viongozi wa upinzani inaodai walishiriki katika kumuapisha
Odinga kuwa anachokitaja Rais wa watu.
Viongozi watatu wa muunganow a upinzani NASA, wabunge TJ Kajwang na Geroge Aladwa pamoja na wakili Miguna Miguna walikamatwa.
Wote waliachiliwa kwa dhamana ili Miguna anasalia kizimbani licha ya
mahakama kuu kuamrisha aachiliwe na anatarajiwa kufikishwa tena
mahakamani Leo.
Katika mkutano wa hadhara jijini Nairobi siku ya Jumapili viongozi wa
upinzani wameapa kufanya maandamano iwapo Miguna hataachiliwa huru
'Ikifikia kesho kama Miguna Miguna hajaachiliwa.. Wale watu wote
tulikuwa Uhuru Park, tutajitokeza twende police station.. tuwe tayari
kushikwa', amesema Godfrey Otsosi kiongozi wa chama cha ANC katika
muungano wa upinzani Nasa Kenya.
Lakini kwa upande wake, serikali imeshikilia kuwa upinzani unakiuka
sheria na hauheshimu uamuzi wa wanachi uliowaweka madarakani.
Makamu wa Rais,William Ruto amesisitiza kuwa hawatafanya mazungumzo na upinzani kuhusu kugawana mamlaka serikali.

No comments:
Post a Comment