Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa
wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo yote ya pwani
kuanzia leo(jana) usiku mpaka Februari 7 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Februari 05, 2018 kutakuwa na
vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi
makubwa yanayozidi mita 2 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya
Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya
Unguja na Pemba.

No comments:
Post a Comment