Kheri Mkono unaotoa kuliko unao pokea.Katika kuadhimisha Miaka 41 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Umoja wa Vijana wa CCM idara ya vyuo na vyuo Vikuu Tawi la Kambarage Saut Mwanza Tuliadhimisha kwa kutembelea hospital ya Butimba kona iliyo wilaya ya Nyamagana katika kitengo cha wazazi waliojifungua.
Kupitia Tawi hilo linaloongozwa na Mwenyekiti wa Tawi DAVIS PETER katibu Bi ELIZABETH NIKILO,na Wajumbe ANYES, KULWA MAHENDA na wanachama wa Tawi letu, tulifanikiwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa wazazi walio kuwepo katika Hospital hiyo.
Zawadi hizo ilikuwa ni vitu mbalimbali kama Sabuni za kufulia,Miche ya Sabuni,kofia za watoto,soksi,nepi n.k
Kama Tawi tulitumia njia hiyo ili Kukiunga mkono Chama Chetu Cha Mapinduzi Chenye kutambua nafasi ya wakina Mama katika Taifa letu.
lakini Pia Kumuunga Mkono Rais wetu Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa Jitihada kubwa Anazofanya na Mama Samia Suluhu Hassan za kuimarisha Amani,Umoja na Upendo kwa Taifa letu kwa kuhakikisha watu wote wanakuwa na Haki Sawa ya kuoa,kuolewa kuzaa, kuishi,kufanya kazi,kuthaminiwa na kuwa na Haki ya kupata Huduma Mbalimbali Kama Afya,Elimu n.k.
Kwa niaba ya wanachama wa Tawi la Kambarage Saut tunawashukuru wadau wote mliojitokeza na kutuunga mkono katika Zoezi hilo kwa kutoa magari yenu,Muda na Nguvu zenu MUNGU Awababariki sana.
TUENDELEE KUKUTANA KAZINI




No comments:
Post a Comment