Serikali imesema Tanzania inazidi kupaa zaidi kiuchuni barani Afrika
baada ya kutajwa na ripoti ya Foresight Afrika iliyotolewa mwaka 2018.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imeshika nafasi ya tano Africa huku
nafasi nne za juu zikishikiliwa na Senegali, Ivory Coast, Ethiopia na
Ghana.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano hii, Msemaji wa Serikali Bw.
Hassan Abbas amesema serikali ya Rais Magufuli imekuwa ikiimarika
kiuchumi kila siku.
“Kwa mujibu wa ripoti ya FORESIGHT AFRICA iliyotolewa mwaka huu (2018)
Tanzania ipo kwenye 5 bora ya nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi barani
Afrika, Ghana ndio imeongoza orodha hiyo kama inavyoonesha,” alisema
Abbas.
Katika hatua nyingne Abbas amesema Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza
kwa utawala bora kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki ikifuatiwa na
majirani zetu Kenya na imekuwa ya 91 duniani.

No comments:
Post a Comment