Thursday, March 8, 2018

KUTOKA IRINGA: JESHI LA POLISI LAANZA UCHUNGUZI TUKIO LA KUTEKWA M/KITI TSNP, ABDUL NONDO

Baada ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi hapa nchini (TSNP), Abdul Nondo aliyepotea usiku wa kuamkia March 7, 20018 katika mazingita kutatanisha,  kuonekana akiwa mkoani Iringa 

 Jeshi la Polisi Mkoani humo limeibuka na kusema limefungua jalada ili kuchunguza mazingira ya upoteaji wa Nondo.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema uchunguzi huo umelenga kubaini kama Nondo alitekwa kweli na watu wasiojulikana au alitoa taarifa za uongo.

Amesema, Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amepatikana akiwa hai na salama bila ya kuwa na mareha yoyote mwilini mwake yanayoashiria alipata mateso.

Kamanda Bwire amesema hadi sasa Nondo bado yupo kituoni hapo wakati uchunguzi unafanyika na kwamba ikibainika alitoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment