Umoja wa vijana wa chama cha mapindizi (UVCCM )mkoa wa mwanza umefanya kikao cha kawaida cha kamati ya utekelezaji. Kabla ya kujadili ajenda zilizokuwa zimeandaliwa katika kikao hicho
Katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa mwanza na mlezi wa jumuiya mwalimu Magwala alianza kwa kutoa nasaha zake kwa wajumbe wa kikao hicho.
Katibu aliwambia wajumbe sasa ni wakati wakujiandaa kikamilifu kupokea na kuyafanyia kazi maelekezo na mabadiliko ya mfumo mpya unao endana na ccm mpya ili kwenda sambamba na kasi ya viongozi wetu wa ngazi ya juu.
Nae mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa mwanza Comrade Jonasi Rufungulo alifungua kikao kwa kuwataka wajumbe kutanguliza maslahi ya jumuiya mbele kuliko kitu chochote.
Umoja ,mshikamano na ubunifu ndio nguzo itakayo leta tija kwenye jumuiya ya vijana ndani ya mkoa wetu .
Mwenye kiti alisisitiza dhamila ya mwenyekiti wa UVCCM Taifa Comrade kheri D James ya kujitegemea kiuchumi na kuondokana na dhana ya kuwa omba omba Kwa kuboresha miradi iliyopo na kubuni miradi mipya ya kiuchumi.
TUKUTANE KAZINI
NAJIVUNIA KUWA MWANA CCM
Katibu hamasa na chipkizi mkoa wa mwanza
Hussein A .Kimu


No comments:
Post a Comment