Kada wa ccm wilaya ya magu, na Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya super sami jina kamili Samson Josiah ameuwawa kikatili na gari yake kuchomwa moto huko serengeti mkoani mara.
Inasemekana kuwa tajiri huyo alitoweka na mawasiliano yake kutopatikana hewani kwa siku takribani nane mpaka jana ambapo mwili wake ulikutwa huko kwenye ifadhi ya pori la serengeti pamoja na gari lake alilokuwa anatumia likiwa limeteketezwa kwa vibaya kwa moto.
Kiukweli inaumiza sana moyo na inachoma mno kwa mauji ya aina hii, Magu tumeguswa sana na msiba huu mzito wa kijana wetu na tunaimani kubwa sana na jeshi la polisi kuwa litachunguza kwa makini tukio hilo ili wausika wapatikane kwa haraka zaidi ili na wao wachukuliwe hatua kali za kisheria ,
R. I. P Brother Josia




No comments:
Post a Comment