Serikali yatenga shilingi billion 5.1 kwaajili ya machinjio yakisasa, Shilingi million 160,000,000 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati, kuanza Kufungua njia za kata ya Mhandu.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana akiendelea na ziara yake kuelekea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2015-2020 Kwa kata zote 18 za halmashauri ya Jiji la Mwanza amewaambia wananchi wa Kata ya Mhandu serikali imetenga shilingi billion 5.1 kupitia miradi ya PP kwaajili ya Machinjio ya hadhi ya kimataifa. Fedha hizi zitakazo nunua machine za takribani shilingi billion 2 na Fedha zingine zitajenga uzio mkubwa wa biashara kwaajili ya vyumba vya Maduka, butcher Kubwa ya kisasa pamoja na ghala Za kuhifadhi mazao ya Nyama ulikuwa na machinjio ya serikali yenye hadhi ya viwango vya kimataifa.
Mhe Stanislaus Mabula amesema kutokana na Kata hiyo kuwa mpya Lakini serikali kupitia mfuko wa Maendeleo halmashauri ya Jiji la Mwanza imetenga shilingi million 160,000,000 pamoja na kutafuta Fedha za fidia zitakazolipwa kwaajili ya uwanja wa kujengea Zanahati hiyo ambayo dhima kuu nikuwa na kituo cha afya. Ujenzi wa Zahanati hii utawezesha usogezaji wa huduma ya afya Karibu na Jamii ili kutekeleza sera ya afya na Ilani ya uchaguzi kila Kata kuwa na Zahanati pamoja na kituo cha afya.
kukabiliana na changamoto ya umeme serikali ya awamu ya tano imejipanga kutoa umeme Nyaguruguru hadi maeneo ya Mhandu
kisiwani.
Ilikufanya usafiri wa barabara kufikika kwasasa haraka tayari halmashauri imejipanga kuboresha barabara zote za Kata hiyo wakati Wote na tayari TAURA itanza na Kata hiyo ya Mhandu Kwanzia ijumamosi Kisha kuelekea kata zingine.
Mwisho mhe Mabula aliwashukuru wananchi kumchangua Diwani mchapa Kazi, msomi mhe Sima anayetokana na Chama Cha Mapinduzi nakuhaidi ushirikiano naye Kipindi chote cha uongozi wake ili kuwaletea wanachi Maendeleo.
Imetolewa na,
Ofisi ya Mbunge,
Jimbo la Nyamagana




No comments:
Post a Comment